Tuesday, May 8, 2012

Taswira ya Elizabeth Micheal mahakamani jana.

Msanii Elizabeth Michael 'Lulu' ambaye ameshitakiwa kwa tuhuma za kumuua Msanii Nguli nchini, Steven Kanumba akiwa chini ya ulinzi mkali wa askari Magereza alipofikishwa tena ,katika Mahakama ya Hakim Mkazi Kisutu, Dar es Salaam.
Lulu anayekabiliwa na kesi ya kumuua mwigizaji mwenzake, Steven Charles Kanumba, kwa sasa anasema ana miaka 17, lakini katika mahojiano kwenye kipindi cha TV cha Mikasi, kabla ya kifo cha The Great aliwahi kusema ana umri wa miaka 18.

Akizungumza mahakamani hapo, Wakili Kaganda alisema mbali na umri wa Lulu kuwa na utata, lakini hata jina lake halisi nalo ni tatizo, pia kwani wakati wengi wanamfahamu kama Elizabeth Michael, lakini cheti chake cha kuzaliwa kinasomeka Diana Elizabeth. 

Katika ufafanuzi wake, Hakimu Mkazi, Augustina Mmbando alisema analitupilia mbali ombi la upande wa utetezi, kwa sababu mtuhumiwa anakabiliwa na kesi ya mauji na imefunguliwa chini ya Kifungu cha 196 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2002.
Alisema kwa mujibu wa kesi hiyo, Mahakama yake haina mamlaka ya kuisikiliza kesi hiyo, zaidi ya Mahakama Kuu. Hakimu Mmbando ameiahirisha kesi hiyo hadi Mei 21, mwaka huu.
 
Tayari msisimko wa kesi hiyo unaonekana kuanza kupungua taratibu, kwani leo Lulu aliwasilishwa katika ulinzi wa kawaida na mahakamani hapo hakukuwa na idadi kubwa ya watu, kama ilivyokuwa alipofikishwa mahakamani mara ya pili, mwezi uliopita. 

9 comments: