Thursday, May 10, 2012

MOTO WATEKETEZA BASI LA KAMPUNI YA MURO INVESTMENT -MOROGORO

Basi la kampuni ya Kampuni ya Muro Investment, T 820 BEY lillilokuwa likitokea Mwanza kwenda jijini Dar es Salaam, limewaka moto na kuteketea kabisa maeneo ya Maseyu Mkoani Morogoro. Ajali hiyo haikusababisha madhara kwa abiria isipokuwa mali zao zote ziliteketea kwa moto huo. chanzo cha ajali hiyo ni hitilafu ya umeme iliyotokea katika gari hilo. Inadaiwa kuwa gari hilo lilipata hitilafu katika taa na walipofika mjini Morogoro walifanyia marekebisho na kuendelea na safari na walipofika maeneo hayo ya Maseyu likashika moto.

0 comments:

Post a Comment