Wednesday, May 2, 2012

Feri yazama India ikiwa na Abiria 300

Takribani watu 103 wanahofiwa kufariki baada ya feri walimokuwa wakisafiria kugongwa na dhoruba Kaskazini Mashariki mwa India.
Polisi wamethibitisha taarifa hiyo, taarifa zinasema kuwa feri hiyo ilikuwa imewabeba abiria 300 wakati ilipopinduka kwenye Mto Brahamaputra katika jimbo la Assam. Taarifa zinasema kuwa watu 100 hawajulikani waliko na kwamba wengine waliokolewa au kujisilimisha baada ya kupinduka kwa feri hiyo.
Kutokana na hali mbovu ya feri nyingi katika eneo hilo kumekuwepo ajali nyingi lakini ajali hii ni mojawapo mbaya zaidi kuwahi kutokea hivi karibuni katika eneo hilo. Maafisa wa polisi wamesema kuwa ajali hiyo ilitokea katika Wilaya Dhubri kufuatia kimbunga kikali. Dhubri ni karibu kilomita 350 kutoka mji mkuu wa Jimbo la Assam wa Guwahati, Polisi walisema feri hiyo ilivunjika vipande viwili kutokana na kimbunga hicho.
"Niliona watu wakisombwa na maji kwa kuwa maji yalikuwa yakienda kwa kasi sana," Mtu mmoja aliyeshuhudia ajali, Rahum Kamarkar

0 comments:

Post a Comment