Saturday, April 21, 2012

Kampuni ya Simu Ya Airtel Yatoa Msaada Wa Compyuta na Vitabu Vyenye Thamani Ya Tsh Mil 25 Kwa Chuo Kikuu Cha Dodoma

Mkuu wa wilaya ya Bhahi Bi Betty Mkwasa, akiwa na Makamu Mkuu wa chuo cha Dodoma (UDOM) jana pamoja na wafanyakazi wa Airtel na baadhi ya wanafunzi wa IT chuoni hapo wakiwa wameshikilia vitabu vilivyotolewa msaada na Airtel kwa chuo hicho wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya vitabu 104 na kompyuta 20 vyote vyenye  thamani ya milioni 25/- TZS  toka Airtel ikiwa ni muendelezo wa Airtel kuchangia sekta ya Elimu nchini.
Chuo kikuu cha Dodoma ambacho ni maarufu kama UDOM kilifunguliwa rasmi mwaka 2007 huku kikiwa  na sifa ya kuwa na maabara kubwa (library) kuliko chuo chochote cha elimu ya juu kilichopo nchini. Kwa sasa chuo hicho kinakadiriwa kuhudumia zaidi ya wafunzi 20,000 nchini huku matarajio ni kufikisha wanafunzi kutoa elimu kwa wanafunzi 40,000 kwa siku zijazo.

0 comments:

Post a Comment