Tuesday, May 1, 2012

Jenerali Ntaganda ateka miji miwili DRC

Vikosi vinavyomtii Bosco Ntaganda, anayetafutwa na ICC vimeteka miji miwili ya mashariki mwa DRC. Mamia ya askari wenye silaha nzito wanaomtii Jenerali Ntaganda hivi karibuni walijitenga kutoka jeshi la nchi hiyo. Akiwa anafahamika kama ''Terminator'', Jenerali Ntaganda amekanusha tuhuma za ICC kuwa aliwasajili watoto kuwa askari. Kutoka umbali wa kilometa 30 (18 maili) magharibi mwa Goma, wakazi wamesikia mapigano kati ya vikosi vya Jenerali Ntaganda na vikosi vya serikali yakiendelea Jumapili usiku. Askari wa serikali walirudishwa nyuma na kuondolewa katika miji ya Mushake na Karuba, mwandishi wetu anasema, na wamerudi nyuma kwa kilometa 12 mashariki mwa mji wa Sake, ambako wanajikusanya kupambana naye.
Askari hao waasi walikimbia jeshi la Congo lenye ngome yake Goma mapema mwezi huu, idadi kati ya 400-500, kwa mujibu wa vyanzo vya UN na Majeshi ya DRC.

 Bosco Ntaganda ''Terminator'' historia yake kwa ufupi’
  • Alizaliwa mwaka 1973 nchini Rwanda
  • Alikimbilia DR Congo akiwa kijana baada ya mashambulizi dhidi ya kabila la Watutsi
  • Akiwa na miaka 17, anaanza siku za mapigano –akibadilisha kati ya waasi na askari, kote Rwanda na DR Congo
  • Akawa mchezaji wa kujitoa wa tennis
  • Mwaka 2006, alishtakiwa ICC kwa tuhuma za kusajili watoto kuwa askari.
  • Ni kiongozi wa vikosi vilivyofanya mauaji ya Kiwanji mwaka 2008
  • Mwaka 2009, anaujiunga na jeshi la Taifa la DRC na kuwa jenerali.
  • Mwaka 2012, anaasi jeshi na kujitenga.
Katika mapigano mengine katika eneo la kaskazini la Kivu ya kaskazini kati ya majimbo ya Mweso na Kitchanga, maafisa wa jeshi la Congo wamesimamisha shughuli za watu wa Jenerali Ntaganda. Kati ya mwaka 2002-2005, Jenerali Ntaganda alikuwa mkuu wa harakai za kijeshi wa waasi wa UCP wakiongozwa na mbabe wa kivita Thomas Lubanga – ambaye mwezi Machi alikuwa wa kwanza kukutwa na hatia na mahakama ya ICC baada ya kukutwa na hatia ya kusajili watoto kuwa askari. Jenerali Ntaganda mtuhumiwa mwenza – lakini Rais Joseph Kabila awali alikataa kukamatwa kwake kwa ajili ya amani ya DRC.
Rais mapema mwezi huu alitoa wito wa kukamatwa kwake lakini anasema hatampeleka ICC. Licha ya kumalizika kwa vita vya DRC mwaka 2003, makundi kadhaa yenye silaha bado yanazunguka katika eneo lenye utajiri mkubwa wa madini mashariki mwa nchi licha ya UN na Jeshi la nchi hiyo kuwanyang’anya silaha.

0 comments:

Post a Comment