Friday, April 27, 2012

Historia ya Charles Taylor

Bw Taylor ndiye kiongozi wa kwanza kutoka Afrika kukabiliwa na hukumu mbele ya Mahakama ya Kimataifa tangu kesi maarufu za Nuremburg baada ya vita vikuu vya pili vya Dunia. Atahukumiwa mwezi ujao.
Charles Taylor alikua Rais wa Liberia kuanzia mwaka 1997 hadi alipojiuzulu mnamo mwaka 2003 kufuatia shinikizo kali za kimataifa. Alianza shughuli za siasa wakati wa ziara yake nchini Liberia kama kiongozi wa msafara wa mashirika ya Waliberia yaliyo barani Amerika mapema katika muongo wa 1980, mapinduzi ya kijeshi yalipofanyika naye kupewa kazi katika serikali ya Samuel Doe.
Baada ya kuteuliwa kama Naibu waziri katika Wizara ya biashara ya serikali ya Rais Doe, Taylor aliikimbilia Marekani kufuatia madai kwamba amepoteza takriban dola za kimarekani milioni moja.
Alifungwa huko Marekani lakini akatoroka jela katika mazingira ambayo hadi leo bado ni ya kutatanisha. Hatimaye aliunda kundi lake la waasi, lililojulikana kama National Patriotic Front of Liberia, ambalo liliiondoa serikali ya Samuel Doe madarakani.
Taylor ana kipaji cha kua mtu mchangamfu ambaye aliweza kumbadili adui na kumpenda kiasi cha kumfanya kua mfuasi sugu. Kwa mfano alipoingia mji wa Monrovia mnamo mwaka 1995 makumi kwa mamia ya watu waliompinga walijitokeza kumpokea na kumuimbia nyimbo za kumsifu kama shujaa.
Licha ya kuwateua watu wengi kama washauri wake lakini hiyo ilikua danganya toto'' kwa sababu hakufuata ushauri wao hata siku moja. Mmoja wa washauri wake wa karibu aliwahi kuniambia kua yaliyomfika Taylor yangeweza kuepukika kama angewasikiliza washauri hao.
Taylor alipenda sana kujifananisha na watawala wa enzi ya karne ya kumi na tisa kwa jinsi alivyowazawadia fukara akifahamu kua fadhila zake zitamjengea sifa na kumfaa siku moja.
Akiwa mpenda madaha alifahami vyema nguvu ya vyombo vya habari na jinsi ya kuvitumilia. Kupitia miaka ya 1990 alishiriki mahijiano mengi ya kipindi cha BBC cha Focus on Africa.
Katika kipindi cha kwanza, akiwa ni kiongozi wa kundi la waasi asiyefahamika, alitangaza mpango wake wa kuivamia Liberia.
Miaka michache baadaye, alipodokezewa na mtangazaji kwamba watu wengi wanamuonelea kua muuwaji, alilipuka na kusema ''Hata Yesu Kristu alituhumiwa kua ni muuwaji enzi zake.
Katika mahojiano mengi aliyofanya daima alijitahidi kudhibiti mahojiano ili kutoa sura inayompendeza yeye. Mfano uilipomrushia suali lililomchukiza alijitahidi kulibadili liweze kusikika kwa manufaa yake.
Kama mpiganaji mahiri alijivunia uwezo wake wa kiume na uwezo wa kuzaa watoto wengi. Hakuficha siri yake ya kupenda wanawake, akidokeza wakati mmoja kua kama kiongozi wa Kiafrika ana haki ya hadi wake wanne.
Mwanamitindo Naomi Campbell alihusishwa katika kesi ya Taylor
Wakosoaji wake walipokashifu tabia yake ya uzinzi, alijibu kwa kuwakemea wanaume wanaofanya mapenzi ya jinsia moja na kujibu ''Bora mimi nawapenda wanawake.''
Mnamo mwaka 1996 alidokezea kua angetaka kujaliwa na watoto wengine watano na wote watakua wanaume. Hata hivyo hakujaliwa na ndoto yake hio watoto wake wawili waliofuata walikua wa kike.
Labda kama ishara ya kujiliwaza majaliwa hayo, aliwahi kusema kua kama mzazi anayewapenda wanawe, mume yeyote atakayewaoa wanangu, itabidi akubali watoto wake warithi jina la Taylor liendelee kudumu katika familia

0 comments:

Post a Comment